Kila chama cha siasa kinaposajiliwa huwa na katiba na kanuni zinazokiongoza katika shughuli na harakati zake za kushika dola. Chama Cha Mapinduzi (CCM), tangu kilipoanzishwa mwaka 1977, kimeendelea kuaminiwa na Watanzania kuunda serikali na kuongoza nchi.

Kwa mujibu wa sheria za usajili wa vyama vya siasa nchini Tanzania, chama kinapaswa kutimiza vigezo vifuatavyo:

  1. Kiwe na uwezo wa kufanya kazi katika pande zote za Muungano.

  2. Kisiwe na itikadi ya dini au dhehebu.

USAJILI WA VYAMA VYA SIASA

Kuna aina mbili za usajili wa vyama vya siasa:

👉Usajili wa muda

👉Usajili wa kudumu

Kwa mujibu wa Political Parties Act, CCM ni chama cha siasa chenye usajili wa kudumu.

MISINGI YA CCM

Kwa mujibu wa historia yake, CCM kiliasisiwa kutokana na vyama vya wakulima na wafanyakazi, ambavyo ni TAA, baadaye TANU, pamoja na ASP. Asili ya vyama hivi ilikuwa ni kutetea maslahi ya wakulima na wafanyakazi.

Misingi ya CCM ni:

👉Utu

👉Udugu

👉Usawa

👉Kujitegemea

Haya yote yalisisitizwa katika Azimio la Arusha la Ujamaa na Kujitegemea.

TUZIFAHAMU NGUZO ZA CCM

1. Demokrasia ya ndani ya chama

Kila baada ya miaka mitano, CCM hufanya uchaguzi wa viongozi kuanzia ngazi ya mashina hadi taifa. Hali hii huimarisha misingi ya chama.

2. Jumuiya za chama

CCM ina jumuiya kuu tatu:

👉Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT)

👉Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM)

👉Wazazi

Jumuiya hizi zimekuwa nguzo muhimu katika kusimamia miradi, kueneza itikadi ya chama, na kuwafikia wananchi wa makundi mbalimbali.

3. Itikadi na falsafa ya kujitegemea

CCM inaamini katika kujitegemea kama taifa na kama chama. Ina uwezo wa kujiendesha kiuchumi na kiutawala kupitia vyanzo vyake vya mapato na michango ya wanachama.

4. Utekelezaji wa ilani ya chama

Kupitia kamati za siasa kuanzia ngazi ya kata hadi taifa, CCM hufuatilia utekelezaji wa miradi ya serikali kama ilivyoainishwa kwenye ilani yake.

5. Taasisi za mafunzo ya itikadi

CCM ina taasisi za mafunzo ya uongozi na itikadi, pamoja na ushirikiano na vyama rafiki kama FRELIMO na ANC. Mfano wa taasisi hizo ni:

👉Chuo cha Ihemi, Iringa

👉Chuo cha Uongozi Kibaha

Kupitia taasisi hizi, chama hupata viongozi wenye weledi na wenye msimamo imara.

6. Mtandao wa mabalozi wa mashina na maskani

CCM ina uwakilishi wa viongozi kuanzia mashina hadi taifa. Mabalozi hawa ni wafuasi wa kujitolea wenye uelewa wa itikadi ya chama, hivyo kuwa nguzo muhimu sana.

7. Ushirikiano wa chama na serikali

Kwa kawaida Mwenyekiti wa CCM Taifa pia huwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hali hii huisaidia CCM kuwa na uongozi imara na mwendelezo wa sera zake.

HITIMISHO

Kutokana na mabadiliko ya teknolojia, mfumo wa kupata kadi za uanachama sasa unafanyika kidijitali. Hali hii imefanya baadhi ya watu kujiunga bila kuelewa vizuri itikadi na falsafa ya CCM.

Ni vyema kuwepo mfumo ambao kabla mwanachama hajapata kadi, apatiwe mafunzo ya msingi kwa njia ya mtandao, ajibu maswali, ndipo aruhusiwe kusajiliwa rasmi.

Tukumbuke kuwa CCM ni chama chenye itikadi, imani na falsafa zake. Hivyo ni muhimu kila anayetaka kuwa mwanachama apitie mafunzo maalum ili awe na uelewa sahihi wa chama.


MAKALA HII IMEANDALIWA NA:
John Francis Haule
Mkuu wa Soko la Samunge
Jiji la Arusha
0756717987 / 0711993907